MWENYEKITI wa kamati ya Mipango miji na Mazingira Manisipaa ya Dodoma Stephen Mwanga Amesimamisha ujenzi wa vibanda vya wafanya Biashara ndogondogo [machinga] katika stend ya Daladala ya Jamatini baada ya kutolidhishwa na Ugawaji wa nafasi zao.
Machinga hao wamesimamishwa kujenga
siku ya kwanza tangu stend hiyo kuanza kutumika baada ya kufungwa
mwaka mmoja uliopita ili kupisha ujenzi utakaokidhi haja ya watumiaji
wa magali hayo yanayotoa huduma za usafiri wa ndani ya mji huo.
Mwenyekiti huyo aliwataka kusimamisha
zoezi hilo la ujengaji wa vibanda vya biashara zao kutokana na kile
alichosema ugawaji ugawaji wa nafasi hauzingitia utarabu kutokana na
viongozi wa machinga hao kupewa jukumu la kusimamia.
Mwanga aliongeza kuwa alifika eneo hilo
kutokana na kusikia malalamiko ya baadhi ya machinga kulalakia
kutotendewa haki wakati zoezi la ugawaji likiendelea kwakuwa wengi
wao walijikuta wakiwekwa pembeni tofauti na walipokuwa kabla ujenzi
huo haujaanza Augost 2012.
Alisema alipofika na kujionea
kilichokuwa kikiendelea Stend hapo aliamua kumjulisha mkurugenzi hali
halisi na hivyo kuamuliwa zoezi la ujenzi na uwekaji wa vibanda
lisimamishwe na kamati ndogo iundwe ili ikutane na uongozi wa
manispaa ili walijadili na kuliweka sawa swala hilo.
'' Nimesimamisha ujezi usiendelee kwa
sababu mtu akishajenga kumuondoa inakuwa ngumu, mimi na kamati yangu
ya mipango miji na mazingira tutakutana na Meya na Mkurugenzi wa
manispaa ili tulitatue swala hili kwa pamoja na kamati yao mapema
iwezekanavyo ili Abiria waendele kupata mahitaji yao kama kawaida'',
alisema Mwanga
kwa upande wao baadhi ya Machinga hao
walisema viongozi wamejilimbikizia nafasi zaidi ya moja kwa kutumia
majina tofauti mpaka ya wake zao huku sura nyingi mpya zikipenyezwa
hata wakati staend hiyo kabla ya kuhamishwa hawakuwepo huku nafasi
hizo zikibanwa kuwa ndogo na wao kujipendelea nafasi za mwanzo.
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara hao
wadogo wadogo Haji kulaya alisema mpangilio huo wa viongozi hauwezi
kubadilishwa kutokana na ramani ya stand hiyo kubadilika kuwa
tofauti na ilivyokuwa mwanzo hali iliyofanya kuwe na mpangilio mpya
katika ugawaji.
![]() |
| majina yakisomwa |
![]() |
| uvunjaji wa mabanda |
![]() |
| nahama na banda langu |



Comments
Post a Comment