Moto mkubwa umezuka katika msikiti wa manyema uliopo
barabara ya saba manispaa ya Dodoma na kusababisha uaharibifu wa sehemu ya jingo
hilo pamoja na samani mbalimbali.
Mashuhuda wa Tukio hilo waliambia BOMALOG RADIO kuwa baada
ya kuswali swala ya ijumaa na kuondoka walishtukia moshi mkubwa ukisambaa
kutokea juu ya msikiti huo.
Walisema baada ya
kuona hivyo waliamua kuwajulisha kikosi cha zimamoto kwa kutumia simu zao na
baada ya muda mfupi walifika na kuanza kuzima Moto huo uliokuwa ukisambaa kwa
kasi kuanzia juu ya ghorofa ya msikiti huo.
Mmoja waumini hao
alietambulika kwa jina moja la Said alisema waliona moto huo ukianzia juu kwenye maungio ya umeme sehehemu ya main switch ambapo uliendelea kusambaa kabla ya kudhibitiwa na kikosi cha zimamoto.
Kamanda wa upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Dodoma
Damas Nyanda aliyefika na kujionea hali halisi alisema walikuwa bado hawajapata
taarifa kama kulikuwa na mtu yeyete aliyejeruhiwa ama kupoteza maisha.
Alisema mpaka wakiti huo walikuwa wanaendele na zoezi la
uokoaji na baada ya mambo yate kuhakikiwa taarifa rasmi ya hasa iliyopatikana
baada ya tahimini ya viongozi wa msikiti huo.
Kwa upande wake mkuu wa kikosi cha zimamoto mkoa Sajenti
Amiry Issa alisema walifika Dakika 4 baada ya kupokea Taarifa ya ajali hiyo ya
Moto na kukuta moto umesamba maeneo mbalimbali ya msikiti huo wenye ghorofa moja.
Issa alisema urahisi wa kuzima moto huo ulitokana na wao
kupewa taarifa mapema kabla ya moto kusambaa sana na kuwa na madhara makubwa.
Akatumia fursa hiyo kuwataka watu kutofanya juhudi za
kuzima moto wowote unaojitokeza wenyewe kabla ya kuwajulisha zimamoto, maana
kwa kufanya hivyo kunachelewesha uzimaji na kusababisha hasara kubwa
BOMALOG RADIO ilishuhudia Mazuria yanayotumiwa kuswali,
vitabu, kanzu na nafaka iliyokuwa ghorofa ya juu kuwa imeunguzwa na moto huo
uliozuka kuanzia majira ya saa 8. 10 mchana.
Comments
Post a Comment