MWENDO kasi wa 140 aliokuwa akiutumia Dereva wa Basi la Al sayd Expess ulisabisha vifo vya zaidi ya watu 6 akiwemo yeye na dereva wa lori alilogongana nalo na wengine 17 kujeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa .
Ajali hiyo iliyotokea katika kijiji cha chinangali 2 wilayani Chamwino mkoani Dodoma wakati basi hilo lenye lililokuwa likitokea Dar es saam kuja mkoani hapa lilipogongana uso kwa uso na lori hilo lenye namba za usajili T102 CGR aina ya Layland Daf lilikuwa na tera.
namba za usajili T 433 DLR
moja wa majeruhi wa ajali hiyo Juma Yusuph 31 mhehe mkazi wa Chidachi manispaa ya Dodoma alisema mwendo huo ulibadilika na kuwa mkubwa kuanzi walipotoka mkaoni Morogoro kiasi cha kufikia kasi hiyo.
‘’Mimi nilikuwa nimekaa mbele karibu na dereva nilipochungulia nikaona speed inasoma 140 huku jamaa akiyapita magali ya mizigo zaidi ya 4 kwa pamoja kama unavyoona mimi nimevunjika mguu lakini siwezi kusema moja kwa moja kuwa Yule dereva ni kama alipanga kujiua na kweli nilishuhudia baadhi ya viungo vyake mbele ya lori’’, alisema yusuph.
Majeruhi wa ajali hiyo ambao wengi wao walivunjika viungo vikiwemo miguu na mikono walisema mwendo mkubwa uloanza baada ya kutoka Morogoro
Kaimu kamanda wa polisi mkoa Damas Nyanda aliwataja majina waliopoteza maisha mbele ya wandishi wa habari kuwa Dereva wa lori Hassan Mohamed umri kati ya 30,35, Ahmed Said, Husen Rajab, Imran Sharif wakazi wa Dar, na Dereva wa Basi hilo Nizar Akran Khan mkazi wa Mpwapwa wakati mwili wa marehemu mmoja bado haujatambuliwa.
Kaimu kamanda huyo alisema Alisema Miili ya maremu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma na wengine 17 waliojeruhiwa kulazwa wakiwemo 7 wanawake na wanaume 10
Nyanda alisema chanzo cha ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 2.30 usiku wa juzi jumapili ni Mwendo kasi wa Dereva wa Basi hilo ambapo ashindwa kulimudu wakati akijaribu kusimama ili kujaribu kujiepusha na ajali hiyo.
Jeshi hilo la polisilimetoa wito kwa watumiaji wa barabara kuwa waangalifu wanapokuwa barabarani huku wakiwa na tahadhari ya kujua kuwa kuna watumiaji wengine.

Comments
Post a Comment