WAKAZI wa kata ya Segara Wilayani Chamwino mkoani Dodoma
wamelalamikia kukosekana kwa huduma ya mawasiliano hali inayowafanya kukosa
huduma za msingi kwa wakati ikiwemo kuuza mazao kwa bei yahasara.
Wakazi hao waliitoa kauli hiyo katika kijiji cha Malechala
walipokuwa kwenye Tambiko la kimila lilihudhuliwa na makabila mbalimbali
yaliyoongozwa na Wanguu toka mkoani Tanga lililohudhuriwa na watu zaidi ya 400
na kufanyika katika himaya ya Fundi Shabani Waziri
mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho Asha Mohamed alisema kumekuwa na kelo ya ukosefu wa
mitandao ya mawasiliano tangu ilipoanzishwa hapa nchini hali ambayo imekuwa
ikiwasababishia kukosa kila huduma za kijamii kwa wakati.
Alisema kutokana na kata hiyo kuwa mbali na makao makuu ya
wilaya hiyo ya Chamwino wamekuwa wakipata taabu ya utoaji wa taarifa za matukio
mbalimbali zikiwemo za ajali, ujambazi, wizi, wagonjwa wanaohitaji huduma za
haraka pia wameshindwa kujua wakati mzuri bei za mazao.
Asha aliongeza kuwa katika vijiji vya Dabalo, Izava,
Chiwondo, Mapange, Magungu na ikombo vinavyojishughulisha na kilimo cha Ufuta,
Karanga, Alizeti na Mahindi kwa ajili ya biashara ambayo wamekua wakisafirisha
kupeleka Dodoma na Arusha kufuata japo mara nyingi wamekuwa wakikuta bei zipo
chini kutokana na kuondoka bila mawiliano.
“Tumekuwa tukipata taabu sana hasa tunaposafirisha mazao
mara nyingi tumekuta bei zipo chini kutokana na ukosefu wa mawasiliano, kama
tungekuwa na mawasiliano tungejua mapema kama zipo chini na ingekuwa hiyali mtu
kusafirisha,
Hapa tulipo unaona mlima ulee km 1 ndipo pana mawasiliano tena ya mang’amng’am
maana ukipata hutakiwi hata kugeuka maana yanakata, usiku umelala linatokea
jambo huwezi kupiga simu ndani mpaka ufike kule hivi kweli viongozi hawaoni au
wao kwa sababu hawaishi huku vijijini?’’, alihoji Asha
Aidha alisema wakazi wote wa kata hiyo wanapotoka nje ya
kata hiyo ndipo huonja radha ya mawasiliano bila bugudha kwani pamoja na wengi
wao kuwa na simu tena za gharama wamezigeuza kuwa radio kaaseti za kuchezea na
kusikilizia miziki.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji hicho cha Malecela
Nganiki Sailepu alisema Ukosefu wa mitandao ya mawasiliano kwa njia ya simu
limeigharimu kata hiyo kwa kipindi kilefu, ambapo pamoja na juhudi za
kumfikishia Mbunge wao wa jimbo la chilonwa Hezekiah Chibulunje na viongozi wa
Wilaya hiyo wamishia ahadi zisizotekelezwa.
Sailepu alisema kuanzia wapewe ahadi hiyo mpaka sasa ni
zaidi ya miaka 4 hakuna lolote ambalo limefanyika badala yake wamekuwa
wakipigwa Danadana na kila kiongozi wa wilaya anayekanyaga kata hiyo ambayo
inategemewa kwa kiwango kikubwa kwa kilimo cha mazao ya Chakula na Biashara
mkoni Dodoma.
| Waganga hao wakiche moja ya ngoma za Kinguu wakati walipokuwa wakijiandaa kuanza tambiko rasmi |
| Waganga wa Tiba za jadi na Ukunga wakiongozwa kuimba na kucheza Ngoma aina ya Ng'anga ambayo huchezwa juu ya kilingo kama ishara ya kupandishwa vyeo walipokuwa wakimalizia Tambiko la kijadi lilifanyika kwenye himaya ya Shabani Waziri, lililofanyika kijiji cha malecela wilayani Chamwino. |
| WAGANGA NA TUNGULI |
Comments
Post a Comment