MWANAMKE wa mwanajeshi aomba msaada kwa wasamalia wema ili
aweze kuwahudumia watoto wake kwa chakula mavazi na elimu kutokana na ugumu wa
maisha kiasi cha kushindwa kupata hata lishe ya kuwapa mapacha watatu
aliojifungua kinyume na matarajio yake.
Mwanamke huyo Rehema Khamis [30] mkazi wa mkalama kata ya
makulu manispaa ya Dodoma aliomba msaada huo baada ya kuona toka ajifungue
watoto hao watatu imefika wakati ameshindwa kuwapatia hata uji wenye lishe huku
mshahara wa Mumewe ukiishia kwenye madeni.
Rehema alisema alijifungua
watoto hao wa kiume wawili na wa kike mmoja Hassan, Husen na Hasanati katika
hospitali ya Rufaa ya Dodoma na sasa wanakaribia kuwa na umri wa mwaka mmoja
aliowachisha kunyonya wakiwa na miezi 7 kutokana na kukosekana maziwa.
Alisema hakutarajia kupata watoto watatukwa mpigo kutokana
na tayali alishakuwa na wengine wawili hivyo alijua akipata mmoja angepumzika
kuzaa ili ajipe nafasi ya kuwalea, hivyo kutokana na watoto hao kuhitaji
chakula, mavazi na hata elimu kwa hao wakubwa imekuwa ni sababu ya kuhitaji
msaada.
‘’Watu wa kada mbalimbali wamekuwa wakifika kuwaona watoto
hawa lakini ni kama uwanja wa \maonyesho na kutaka kuniona mama yao
wakishatuona wanaondoka lakini si kwa kuleta msaada wowote hivyo naomba wenye uwezo
na moyo wanisaidie ili niweze kuwapa malezi bora’’,alisema Rehema.
Nae Baba wa watoto hao Abubakari Ally Hamad Mwanajeshi wa
ajira mpya katika jeshi la wananchi wa Tanzania [JWTZ] kikosi cha 673 Msalato
Dodoma alisema mahitaji yamekuwa hayatoshelezi kutokana na mshara anaopata
kuishia kwenye madeni ambayo amekuwa akikopa kwa wanajeshi wenzake.
Alisema pesa hata madeni hayo ambayo amekuwa akikopa
hayatoshelezi mahitaji ya watoto hao ambao hata hivyo hahitaji kuongeza
wengine, hata hivyo aliwataka watu mbalimbali zikiwemo taasisi za kiserikali
kumsaidia kutokana na watakavyojaliwa na mwenyezi mungu ili aweze kuwa tunza
watoto wake.
Kwa upande wake Ofisa mtendaji wa kijiji cha makulu Namsfu
Mihungo alisema wao kama serekali wanajitahidi kufikisha ujumbe kwa watu kuhusu
familia hiyo kuhitaji msaada na kufika kuwaona lakini hawakujua kama hakuna
msaada unaotolewa, hivyo watajipanga kuona nini watafanya ili kuisadia familia
hiyo kwa kadili watakavyoweza.
![]() |
| Watoto Hussen, Hassan na Hasanati waliozaliwa mapacha watatu ndivyo wanavyoonekana wakiwa wamebakiza siku chache kutimiza mwaka tangu wazaliwe. |

Comments
Post a Comment