PIKIPIKI zinazotolewa kwa jeshi la polisi mkoani Dodoma na
wahsani mbalimbali ni kwa ajili ya kuwahi matukio hazitolewi kwa ajili ya
matumizi ya nyumba ndogo za askari.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Lephy Gembe alipokuwa akizindua Mradi wa polisi Jamii unaojulikana kama ZONE TASK FORCE iliyohusisha mjini, Zuzu na kikombo
Mkuu huyo wa wilaya alisema pikipiki hizo zinatolewa kwa lengo maarumu la kuwahi kwenye matukio pondi polisi wanapopata taarifa ya uhalifu unafanyika au unaopangwa kufanyika mahali na si za kutembelea au kuendea kwenye nyumba ndogo.
Aidha Gembe alisema vikosi kazi vya tarafa [TASK FORCE] ,ambavyo lengo lake kuu ni kuendeleza na kusimamia shughuli za ulinzi na usalama wa tarafa hizo kwa kuzingatia sera ya ushirikishwaji wa jamii
Aliongeza kuwa mpang o huo wa uzinduzi wa tarafa , vikosi kazi pamoja na shughuli za polisi jamii ni kuhakikisha kuwa makosa yanayoweza kujitokeza katika tarafa ambayo yanaweza kuwafanya wananchi wetu wasifanye mambo ya maendeleo yao kiufanisi yanaondolewa kabisa katika jamii.
Awali akizungumza kwenye uzinduzi huo kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa Damas Nyanda alisema lengo kuu la uzinduzi huo ni katika kuendeleza, kuimalisha ulinzi na usalama nchini, katika kutekeleza mpango mkakati wa kuweka askari wasiopungua 15 kwa kila Tarafa.
Katika uzinduzi huo ambao jeshi hilo lilikabidhiwa pikipiki tatu zilizotolewa na Benk ya NMB na moja kamanda wa jeshi hilo David Miseme, huku mdau mwingine wa ulinzi shirikishi Diwani wa kata ya Tambukareli Adamu Perugina alikabidhi mizinga 50 kwaajili ya ufugaji wa nyuki kwa ajili ya vijana kiuchumi wanaoendelea na polisi jamii.

Comments
Post a Comment