WAKAZI wa kijiji cha nagulo wameonywa kutopitisha mifugo yao katika
barabara bila mpangilio maarumu uliowekwa na uongozi wa kijiji hicho la
sivyo watatozwa faini kali.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi [CCM wilayani
Bahi Mkoani Dodoma Philemon Mdate alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea
miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo.
Mwenyekiti huyo alisema kumekuwa na upitishaji holela wa mifugo katika
maeneo mengi ya barabara wilayani humo hali ambayo imekuwa ikichangia
uhalibifu mkubwa ikiwemo mashimo huku usalama wa mifugo yenyewe ukiwa
hatarini.
Mdate alikuwa akisisitiza hilo mara baada ya kumaliza kuitembelea
barabara iliyomalizika
kujengwa katika kijiji hicho cha nagulo kwa yenye ulefu wa KM. 6 kwa
kiwango cha changalawe, huku akiwataka afisa mtendaji na Mwenyekiti wa
kijiji hicho kuhakikisha wanatenga na ijengea kuwa njia pekee ya kupitishia
mifugo.
‘’Ili kuepusha uhalibifu wa barabara mwenyekiti na mtendaji tengeni eneo na
mlijenge ili mifugo yote ipitishwe hapo na mtu yoyote atakaekiuka atatozwa
faini isiyopungua 5000 kwa ng’ombe mmoja na mbuzi mmoja 2500 na msiwe na
huruma kwa mtu’’, alisema
Aidha aliwataka wananchi wote wa kijiji hicho kuilinda barabara hiyo
kutokana na kujengwa kwa gharama kubwa ya 71.6 milioni, hivyo watoe
ushirikiano wa kutoa taarifa kwa viongozi wao.
Katika ziara hiyo Mwenyekiti huyo wa CCM Bahi alitembelea miradi mingine
ya Afya, Elimu na ofisi ya serekali ya kijiji iliyojengwa kutokana na nguvu
na gharama za wakazi wa kijiji hicho.

![]() |
| Barabara hiyo iliyomalizika kuchongwa kwa
kiwango cha Changalawe inavyoonekana baada ya kukamilika |
| Pamoja na mwenyekiti huyo kupiga marufuku mifugo
kutokatiza barabara hiyo bila utaratibu mbuzi wanapita wakati hata hajamaliza kuikagua barabara hiyo iliyo katika kiwango cha changalawe. |

Comments
Post a Comment