![]() |
| Asikari wa wasalama barabarani akisaidiana kupima upana wa barabara sehemu ilipotokea ajali hiyo ilihusisha pikipiki na lori la mizigo. |
WANAFUNZI wawili wa chuo cha biashara (CBE ) wamepoteza maisha papo hapo
kwenye ajali baada ya kugonga tela la mizigo lililokwama barabarani
baada ya kuharibika.
Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 1.00 usiku baada ya kugonga tela
la lori la mizigo kwa nyuma wakati wanafunzi hao walipokuwa wakitokea
kwenye mwaliko wa sherehe ya rafiki zao iliyofanyika katika kijiji cha
ihumwa manispaa ya Dodoma.
Bomalog ilishuhudia msongamano mkubwa wa magari katika barabara hiyo
iliyopo pembezoni mwa kambi ya jeshi ya Ihumwa kwa takribani saa zaidi
ya tatu kabla ya polisi wa usalama barabarani kufika na kuongoza
utaratibu wa kuondoka.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Suzan Kaganda alisema chanzo cha
ajali hiyo ni mwendo kasi wa wanafunzi hao wakati wakiendesha pikipiki
hiyo yenye namba za usajili T 420 CCN waliokuwa wakukitokea barabara
ya morogoro kuingia mjini.
Suzan aliwataja kuwa ni Ramadhan Lesso na Gerger Lwandala wanafunzi wa
CBE na kwamba uzembe wa Dereva wa lori hilo lenye namba za usajili T
477 ABM na huku Tela lake ni T 838 AAZ aliyeliacha barabrani zaidi ya
wiki bala kuweka alama yoyote huku matengenezo ya barabara hiyo
yakiendelea katik eneo hilo.
Aliongeza kuwa miili ya marehemu hao iliyokuwa imehalibika vibaya
kutokana na kufumuka fuvu la kichwa cha aliyekua dereva wa pikipiki hiyo
na ubongo kusambaa katika eneo hilo imehifadhiwa katika hospital ya
mkoa.
![]() |
| Baadhi ya asikari wa Jeshi la wananchi walionekana kujaribu kutoa msaada katika ajali hiyo iliyosababisha vifo vya wanafunzi wa chuo cha biashara CBE Dodoma. |





Comments
Post a Comment