Aliyekuwa ofisa mwandamizi wa benki ya Stanbic tawi la
Tanzania, Shose Sinare amehusishwa na mipango ya kifisadi ambayo
imeisababishia Serikali ya Tanzania hasara ya Sh1.3 trilioni kati ya
mwaka 2012 na 2013.
Taarifa ambazo
gazeti hili limepata kutoka Uingereza na hapa nchini, mwanadada huyo ambaye alikuwa mrembo wa Tanzania mwaka 1996, alishirikiana na aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bashir Awale.
gazeti hili limepata kutoka Uingereza na hapa nchini, mwanadada huyo ambaye alikuwa mrembo wa Tanzania mwaka 1996, alishirikiana na aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bashir Awale.
Sinare hakupatikana kufafanua suala hilo ilhali Awale alifukuzwa nchini hivi karibuni.
Alipoulizwa jana kuhusu tuhuma hizo, Mkurugenzi Mkuu wa
Takukuru, Dk Edward Hosea alisema anatambua suala hilo, linafuatiliwa
na taasisi yake na hakutaka kutoa maelezo zaidi.
Taarifa kwamba Serikali imetumbukia katika kashfa nyingine
kubwa ya ufisadi zimebainika baada Taasisi ya Uchunguzi wa Makosa
Makubwa ya Ufisadi ya Uingereza (SFO) kuwasilisha mahakamani ushahidi
wake kwamba kiasi cha Sh1.3 trilioni kilipotea wakati wa uuzwaji wa hati
fungani za Serikali kwa benki ya Stanbic inayomilikiwa na Standard
Group ya Afrika Kusini.
Mwanasheria wa SFO, Edward Garnier aliiambia Mahakama ya
Southwark Crown ya jijini London, Uingereza inayosikiliza shauri hilo la
kibiashara kwamba wakati wa mchakato wa benki kununua hati fungani
Awale na Sinare walihusika.
Garnier alisema Awale alifukuzwa kazi Agosti 2013 baada ya
kushindwa kutoa ushirikiano kwa timu ya uchunguzi ya ndani na Sinare
alijiuzuru Juni 2013 na hivyo naye alifanikiwa kukwepa uchunguzi.
Katika uchunguzi huo, Garnier alisema maofisa hao
waliwataka maofisa wa Serikali ya Tanzania wawapatie kwanza kiasi cha
Dola za Kimarekani 6 milioni (Sh13 bilioni) ili waweze kufanikisha mkopo
wa Dola 600 milioni (Sh1.3 trilioni) na ziingizwe kwenye akaunti za
maofisa binafsi wa Serikali. Dola 6 milioni ni asilimia moja ya mkopo
huo wa Dola 600 milioni. Garnier alisema mpaka sasa hakuna anayefahamu
fedha hizo zipo mikononi mwa nani.
Hii ni mara ya pili SFO inafanikiwa kuibua ufisadi wa
mabilioni ya dola kwa maofisa wa Serikali ya Tanzania baada ya ule wa
mwaka 2002 ambapo maofisa waliongeza Sh73 bilioni katika bei halisi ya
rada kutoka kampuni ya vifaa vya kijeshi ya Uingereza ya BAE Systems.
Watanzania walipopata habari hizo walipiga kelele maofisa
waliohusika wachukuliwe hatua lakini Serikali ilikataa. Baadaye
yalifanyika makubaliano maofisa wasishtakiwe na BAE pia isishtakiwe,
lakini fedha zilirejeshwa nchini.
Katika shauri hili yanataka kufanyika makubaliano kama hayo
ya awali kwamba Stanbic inayonilikiwa na kampuni ya Standard Group ya
Afrika Kusini ambayo ni kampuni tanzu ya Industrial and Commercial Bank
of China (ICBC) inatakiwa kulipa Dola 32.2milioni sawa na Sh69 bilioni,
ikiwa ni pamoja na kuwalipa SFO Dola 16.0 milioni sawa na Sh36.3
bilioni. Pia inatakiwa kulipa faini ya Dola 6 milioni (Sh12.9) na riba
Dola 1 milioni (Sh2.1bilioni) kwa Serikali ya Tanzania.
Zitto Kabwe
Akizungumzia sakata hilo, Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo,
Zitto Kabwe aliitaka Serikali kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo
vya sheria wote waliohusika na ufisadi huo. Zitto, kupitia taarifa kwa
vyombo vya habari aliyoitoa jana alisema kati ya mwaka 2012/2013,
Serikali kupitia Wizara ya Fedha iliuza hati fungani zenye thamani ya
kiasi hicho cha fedha, ambapo dhamana za Serikali zilinunuliwa na benki
ya Stanbic inayomilikiwa na benki ya Standard Group ya Afrika Kusini.
“Hata hivyo, sehemu ya fedha hizo hazikuingia kwenye
akaunti za Serikali ya Tanzania na pia gharama za bond (hati fungani)
hiyo zilipaishwa kupitia wakala wa kati kati (middle men) na hivyo
kupelekea rushwa ya takribani $60 milioni (Sh129 bilioni) kutolewa kwa
maafisa waliothibitisha biashara hiyo,” alisema.
Stanbic
Hii itakuwa mara ya pili benki ya Stanbic kuingia katika
mgogoro baada ya mwaka jana kutuhumiwa kupitisha kiasi kikubwa cha fedha
kilichotokana na mgawa wa Sh306 bilioni kutoka Akaunti ya Tegeta.
Baadhi ya maofisa, mawaziri na watu maarufu waliopewa fedha
zinazoaminika zilitoka Tegeta Escrow kupitia benki ya Mkombozi
walijulikana na wakafikishwa katika Baraza la Maadili, lakini waliopokea
fedha kutoka Stanbic hawajulikani ingawa uchunguzi uliofanywa na
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) aligundua kwamba
watu hao walichukua kwa mifuko ya sandarusi na plastiki.
c,mwananchi

Comments
Post a Comment