MNADA wa pili wa madini ghafi ya Tanzanite umeingiza dola za Marekani 4,202,287.13 baada ya kuuzwa
gramu 990,039.04
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk. Joel Bedera, alisema hayo
katika hafla ya kuwatangaza washindi wa mnada wa madini hayo yaliyofanyika
jijini hapa juzi.
“Inashangaza hivi sasa wachimbaji kuwapo urasimu katika
kununua baruti kwa ajili ya uchimbaji wa madini, kwanini shirika moja tu la
Mzinga ndilo liuze baruti hali inayosababisha ukata wa madini aina ya
Tanzanite, ni kitu cha kushangaza katika zama hizi za utandawazi kuona biashara
inamilikiwa na mmoja tu na kupelekea mateso kwa watumiaji wa bidhaa za baruti
kwani wataalam wa migodi wanasema madini hayo hivi sasa yanapatikana kwa umbali
mkubwa wa zaidi ya mita 1,000 kwenda chini," alisema.
Hata hivyo, alitoa rai kwa wachimbaji wa madini hayo kuwa
na mpango mkakati wa kuendesha migodi kisasa ili kuwezesha kupatikana kwa
urahisi madini na kupunguza ajali migodini.
Pia aliitaka Wizara ya Nishati na Madini kusimamia
maslahi ya wafanyakazi migodini kwa kushirikiana na idara ya kazi.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, alisema
serikali itakaa na wadau wa madini na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
kuangalia ongezeko la kodi la asilimia 18 wanayotozwa Watanzania
wanaposafirisha madini nje ya nchi, huku mgeni anayenunua madini hayo akitozwa
asilimia 10 ya kodi.
“Kama kweli biashara hii inamnufaisha Mtanzania basi
awekewe mazingira rafiki ya kulipa kodi na kuyauza nchi mbalimbali,” alisema.
Wizara ya Nishati na Madini imefanya mnada wa pili wa
kimataifa wa madini ghafi ya Tanzanite na kampuni 68 zilijitokeza kununua
madini hayo, huku 39 zikiwa ni za wazawa na 29 zikiwa zinatoka nchi mbalimbali
duniani.
Katika mnada huo, kampuni tatu zinazochimba madini ya
Tanzanite za Tanzanite one Mining Company Ltd, Mathias J. Lyatuu Mining na
Tanzanite Africa Ltd zilipeleka jumla ya gramu 990,444.04 za madini ghafi na
gramu 990, 039,04 za Tanzanite ghafi ziliuzwa na kuingiza dola za Marekani
4,202,287.13 sawa na asilimia 99.
Kupitia mnada huo, serikali imekusanya mrabaha wa dola za
Marekani 210,114.36 sawa na zaidi ya Sh. bilioni 466, huku Halmashauri ya
Wilaya ya Simanjiro ikitarajia kulipwa Sh. milioni 27,987,232,.29 kama kodi ya
huduma.
Comments
Post a Comment