SERIKALI inatarajia kupiga marufuku
utengenezaji na uingizaji wa pombe za bei rahisi maarufu kama `Viroba' nchini
ndani ya
miezi mitatu ijayo sawa na siku 90.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Dk. Hamisi Kigwangalla, aliyasema hayo bungeni mjini Dodoma juzi
alipokuwa akijibu hoja za wabunge waliokuwa wakilalamikia kilevi hicho kutokana
na kupunguza nguvu kazi ya Taifa wakati wa uwasilishwaji wa taarifa za Kamati
ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kwa mwaka
2016/17.
Dk. Kigwangalla alisema kuwa baada ya miezi mitatu,
kilevi hicho kitapigwa marufuku kutengenezwa au kuingizwa nchini pamoja na
kuziba mianya yote ya uingizaji.
Alisema kilevi hicho hutumiwa na vijana wengi na hivyo
kuharibu nguvu kazi ya Taifa.
Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini Esther
Matiko, amesema kwamba pombe hiyo inasababisha vifo vya vijana wengi nchini
ambao ndio tegemeo kubwa na nguvu kazi ya Taifa.
“Katika kipindi hiki kifupi cha likizo yangu, nilikuwa
jimboni kwangu na tumezika vijana wanne waliofariki dunia kutokana na matumizi
ya viroba.
Hivyo wananchi wa jimbo langu wameniagiza kuja kulieleza
Bunge athari za pombe hiyo ili tujadili na kuona namna gani ya kuliokoa Taifa
hasa vijana kutoka katika janga hilo,” alifafanua Matiko.
Akiwasilisha taarifa ya Kamati, Mwenyekiti wa kamati
hiyo, Dk. Faustine Ndugulile, alisema kuwa Kamati imebaini uwepo wa uhusiano
mkubwa kati ya matumizi ya pombe hizo na kuongezeka kwa tabia hatarishi
zinazochangia ongezeko la vijana katika matumizi ya dawa za kulevya.
Aidha, alisema hali hiyo
inaathiri ufanisi wa nguvu kazi ya Taifa kutokana na madhara ya matumizi ya
dawa za kulevya.Hivyo Kamati imeishauri serikali kufungia kabisa uzalishaji na uuzwaji wa pombe hizo za viroba ili kulinusuru Taifa

Comments
Post a Comment