Jumamosi iliyopita, IGP Mangu aliwasimamisha askari
waliotajwa kwenye
orodha aliyoitaja Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda wakati
akizungumza na wanahabari hivi karibuni juu ya biashara
hiyo.
*Dar es Salaam.* Rais John Magufuli amempongeza Mkuu wa
Jeshi la Polisi
(IGP), Ernest Mangu kwa kuwasimamisha kazi askari 12 ili
kupisha
uchunguzi kwa tuhuma za kujihusisha na biashara za dawa
za kulevya.
Jumamosi iliyopita, IGP Mangu aliwasimamisha askari
waliotajwa kwenye
orodha aliyoitaja Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda wakati
akizungumza na wanahabari hivi karibuni juu ya biashara
hiyo.
Rais Magufuli ametoa pongezi hizo leo Ikulu jijini hapa
wakati wa
sherehe za kumuapisha Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi,
Jenerali Venance
Mabeyo.
Amesema hatua aliyochukua IGP Mangu inaleta taswira nzuri
kwa Jeshi la
Polisi katika vita dhidi ya dawa za kulevya.
Na: Emmanuel Mtengwa,

Comments
Post a Comment