MSANII wa bongofleva, Khalid Mohamed 'TID'
jana alikiri kwenye
mkutano uliokuwa umeandaliwa na Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam,
Paul Makonda.
Akizungumza katika mkutano huo, TID alikiri kuwa miongoni
mwa wasanii wa muziki huo wanatumia madawa ya kulevya.
‘’Kweli nimekuwa miongoni mwa wasanii wanao tumia madawa
ya kulevya na nimeikosea sana familia yangu na nimewakosea sana mashabiki wangu
hivyo nakiri kuwa sitojiingiza tena katika matatizo haya na nitakuwa mstari wa
mbele kupambana na vita hivi, kwa sasa mimi situmii tena’’, alisema TID
Aidha,TID alimpongeza Rais wa Tanzania, John Magufuli na
Makonda kwa kuanzisha oparesheni juu ya madawa ya kulevya ambayo imechangia kwa
kiasi kikubwa sana kuwahamasisha vijana wengi kuachana na matumizi ya madawa ya
kulevya.
TID mara kwa mara alikuwa akihusishwa na matumizi ya
madawa ya kulevya na alikuwa akikataa kujihusisha nayo mpaka alipotajwa na
Makonda kwenye 'kamata kamata' ya watumiaji na wauzaji wa madawa hayo.
Wasanii wengine walihusishwa na madawa hayo ni pamoja na
Wema Sepetu, Petitman, Recho, Mr blue, Babuu wa Kitaa pamoja na Dogo Hamidu.
Comments
Post a Comment