Baada
ya Watanzania wanaoishi nchini Msumbiji kufanyiwa vitendo vya kikatili na
kufukuzwa, Serikali mkoani hapa imelazimika kuwasafirisha kwa kutumia
magari ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ili kuwafikisha karibu na mikoa
wanakotokea.
Ofisa
Uhamiaji Mkoa wa Mtwara, Rose Mhagama amesema hadi kufikia juzi, Watanzania
waliojisajili katika mpaka wa Kilambo wakitokea Msumbiji walikuwa 220.
Amesema
tayari watu 109 wa awamu ya kwanza wamesafirishwa, ambao waliishukuru Serikali
na wakazi wa Mtwara kwa kuwapokea na kuwapa misaada mbalimbali.
Mmoja
wa waliorudishwa, Mwajuma Abdallah amesema: “Tunawashukuru wanamtwara na
Serikali kwa jumla kwa kutupokea vizuri leo (jana) tunarudi nyumbani.”

Comments
Post a Comment