Dar es Salaam. Askofu wa kanisa la Ufufuo na uzima Joseph Gwajima
amezungumza na waandishi wa habari wa Clouds Media Group na
kusema
kilichomfanya afike katika ofisi hizo ni kutoa pole kwa kuwa yeye ni sehemu ya
sababu za uvamizi huo.
“Isingekuwa
busara watu wavamiwe na mimi ni mhusika mkuu halafu nisije kutoa pole,” alisema
Hatua
ya Gwajima imekuja baada ya tukio la kituo hicho kuvamiwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul
Makonda akiwa na polisi wenye silaha.
Gwajima aliwasili saa 4:00 asubuhi akiwa ameongozana na msafara wa magari zaidi ya manne na
walinzi wake takribani 30 na alipofika alipokelewa na Mkurugenzi wa vipindi na
Uzalishaji Ruge Mutahaba na kufanya mazungumzo na waandishi wa habari na
baadaye na uongozi wa kituo hicho.
Amewataka Clouds kuendelea
na kazi zao za kawaida na kutaka suala hilo
lisichukuliwe kisiasa huku akikisitiza kuwa Mkuu wa mkoa alikosea

Comments
Post a Comment