Aliyekuwa
Waziri Mkuu, Edward Lowassa amesema
anawakaribisha Chadema waliofukuzwa
uanachama baada ya mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM kupitisha uamuzi wa
kuwatimua 12 kati ya 24 walioadhibiwa.
Amesema
walioadhibiwa ni mashujaa waliosimama kutetea demokrasia.
Lowassa
yuko katikati ya tuhuma zilizosababisha wanachama wengi wa CCM kuchukuliwa
hatua baada ya uamuzi wake wa kuhamia Chadema kupinga kuenguliwa kugombea
urais, kufuatiwa na viongozi kadhaa na wanachama kujiondoa chama tawala na
kujiunga na upinzani.
Katika
taarifa yake aliyoituma kwa vyombo vya habari jana, Lowassa ambaye pia alikuwa
mbunge wa Monduli kwa tiketi ya CCM hadi mwaka 2015, amesema viongozi
waliotimuliwa na chama hicho tawala walitumia demokrasia yao kupinga upindishwaji wa kanuni na sheria.
“Hawa
walikuwa mashujaa wa kutetea haki, demokrasia na taratibu na kupinga dhuluma
ndani ya chama chao na nchini,” amesema Lowassa, ambaye kabla ya kuenguliwa
alikuwa mmoja wa makada waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya kupitishwa kuwania
urais kwa tiketi ya CCM.

Comments
Post a Comment