Uzinduzi
wa magari ya kiwanda cha saruji cha dangote mtwara umefanyika leo mjini mtwara
ukiwa umehudhuriwa na
viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo waziri wa nishati na madini profesa muhongo.
viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo waziri wa nishati na madini profesa muhongo.
Raisi
magufuli ameziainisha changamoto kadhaa na ukiritimba uliopo baina ya watendaji
na kampuni zilizo aminiwa ambazo zimeonekana kukwamisha juhudi mbalimbali za
maendeleo ya kiwanda hicho
Raisi
magufuli amemshukuru alhaji dangote kwa uwekezaji wake katika nchi ya Tanzania kwani
kiwanda hicho kimetoa nafasi za ajira za moja kwa moja takribani 800 na jumla
ya ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja ni elfu ishirini
Pia
amemshukuru Raisi kikwete na uongozi wa awamu ya nne kwa juhudi kubwa za
ufanilishaji wa uwekezaji wa kiwanda hicho ambao umewezasha serikali kukusanya
jumla ya mapato ya shilingi bilioni 46 za kitanzania tangu kilipoanza
uzalishaji tarehe 16/2/2016 baada ya kuzinduliwa tarehe 10/10/2015
kiwanda
cha saruji cha dangote kinatarjiwa kudhalisha tani milioni tatu za saruji kwa
mwaka hali itayopelekea ukusanyaji wa mapato wa bilioni 136 kwa mwaka
serikalini
aidha
raisi magufuli amezitaja changamoto zilizopo na zilizokuwepo katika kiwanda
hicho kuwa ni
Magari yalikaa miezi
miwili bandarini baada ya kufika na
yalitoka siku moja baada ya mimi kupiga simu “hivyo nikabaini kuna tatizo hapa” alisema
upatikanaji wa mali ghafi kwa maana ya makaa ya mawe na gesi kwani shirika la
NDC lililopewa dhamana ya uzalishaji wa makaa ya mawe halikufanya kazi yake badala
yake kuingia mkataba na shirika lingine la TAN COAL ili kuchimba makaa ya mawe
ambalo shirika hilo pia limekuwa kikwazo kwa upatikanaji wa mali ghafi za
kutosha kutumika katika kiwanda cha saruji hivyo Raisi magufuli ameamrisha
serikali kutoa kibali kupewa eneo la kuchimba makaa ya Mawe kwa alhaji dangote
ili ili kuondoa hali hii kwa makampuni hayo ambayo ameyaita ni ya kitapeli
aidha profesa muhongo amemuahidi Raisi wa jamuhuri ya muungano masuala hayo kufanyiwa kazi hadi kufikia
jumatano ya wiki ijayo
changamoto ya gesi
kudhalishwa mtwara kisha kusafirishwa
kilomita miatano mpaka jijini Dar-Es-Salaam na kasha kurudishwa tena mtwara
kuuzwa jambo ambalo linaongeza gharama ya malighafi hiyo badala kupatikana
palepale mkoani mtwara kiasi cha kilomita 5 hadi 6
Raisi ameitaja changamoto
ya nafasi za ajira kwa wazawa hasa za udereva kwani kumekuwa na kampuni
nyingine katikati ya upatikanaji wa ajira kiwandani hapo inayofikia kupokea
hata rushwa ili kupata ajira kwa watumishi hali iliyo wasilishwa na mwakilishi
wa madereva aliyepewa nafasi ya kueleza hali ya ajira kiwandani hapo “kwani
ajira za madereva zilitangazwa zaidi ya miatanao tuliitikia wito usaili na
mafunzo ya awali yalitolewa tukisubiri kuitwa hadi sasa hakuna dereva aliyeitwa
kiwanda kinatumia magari ya kukodi baadhi ya watu wameazisha kampuni ili
kufanya kazi” amesisiitiza muhindi
ambaye ana magari zaidi ya miambili ni kama ameanzisha kampuni ya dangote B
ndani ya kampuni inayomilikiwa na hao wanaofanya udalali je wahindi wanafanya
nini Akisitiza wachunguze hata uhalali wa uraia wao Raisi ameahidi suala hilo
kufanyiwa kazi na akielekeza watendaji wake kufanyia kazi maamuzi ya mambo kama
hayo mapema na sio kumsubiri yeye
Raisi amezindua magari hayo yatakayotumika kiwandani hapo
yakitarajiwa kutoa ajira zaidi ya miatano kwa kukata utepe pamoja na alhaji
dangote

Comments
Post a Comment