Dodoma. Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo,
Harrison Mwakyembe, ameondoa zuio la kufungiwa kwa wimbo wa
‘Wapo’ wa
mwanamuziki Nay wa Mitego.
Akizungumza
na waandishi mjini Dodoma leo, Waziri Mwakyembe
alimtaka mwanamuziki huyo auboreshe wimbo huo na ikiwezekana aende Dodoma ili akamuongezee
maneno zaidi.
Kabla
ya kauli ya Dk Mwakyembe ya kuondoa zuio hilo,
Baraza la Sanaa la Taifa(Basata) lilizuia kupigwa au kusikilizwa kwa wimbo huo.
Jana
msanii huyo alikamatwa akiwa Morogoro katika shughuli zake za muziki na kuletwa
jijini Dar es Salaam,
kwa kile kilichoelezwa kuwa wimbo wake umeikashfu serikali.

Comments
Post a Comment