TAIFA la Norway hivi sasa ndiyo kinara wa kuwa na raia wenye furaha
zaidi duniani, taarifa ya kitafiti ya Umoja wa Mataifa inabainisha.
Ripoti inayohusu furaha ya
umma duniani, inabanisha namna
watu wanavyokuwa na furaha na chimbuko lake lilivyo.
Nchi nyingine tano katika orodha iliyoko ni pamoja na
Denmark, Iceland, Uswisi na Finland ambazo ziko katika nafasi nzuri, huku
Jamhuri ya Afrika ya Kati ikiongoza kwa huzuni.
Mataifa ya Ulaya Magharibi na Amerika Kaskazini kwa sasa
yameshikilia nafasi za juu, huku nchi maarufu duniani kama vile Marekani na
Uingereza zikishika nafasi za 14 na 19 kutoka kileleni.
Umoja wa Mataifa unaorodhesha nchi zingine zenye furaha
kama vile Uholanzi, Canada, New Zealand, Australia na Sweden.
Pia mataifa yaliyoko Kusini mwa jangwa la Sahara yako
chini katika maisha ya raia wake kukosa furaha zaidi.
Ripoti hiyo inataja nchi ambayo raia wake wanaongoza kwa
huzuni duniani au kokosa furaha ni Jamhuri Afrika ya Kati.
Zingine vinara katika hali hiyo, ni pamoja na Yemen,
Sudan Kusini na Liberia.
Ni aina ya ripoti inayotokana na maswali ya kitafiti kwa
watu zaidi ya 1,000 kutoka nchi 150 tofauti waliohojiwa ndani ya mwaka.
Miongoni mwa vigezo vilivyotumika ni ukaguzi wa pato la
taifa, huduma za jamii, umri wa kuishi na uwepo wa rushwa.
Pia, ripoti hiyo ya mwaka huu inayojadili furaha ilikuwa
na mada inayoangalia sababu za kushuka furaha nchini Marekani katika siku za
karibuni.
Mkurugenzi wa Mtandao wa Maendeleo Endelevu, Jeffrey
Sachs, anasema kuna shaka kwamba chini ya uongozi na sera za Rais mpya, Donald
Trump, mambo yanaweza kuwa mabaya zaidi.
Wakati Norway iking’ara kwa kuwa na asilimia 75.5 ya
furaha, watu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wako katika wastani wa asilimia
26.9 ya furaha.
26.9 ya furaha.

Comments
Post a Comment