Msanii na muuza nyago kwenye video za Bongo Fleva, Lulu Augen ‘Amber Lulu’.
MSANII na muuza nyago kwenye video za Bongo Fleva, Lulu Augen ‘Amber Lulu’,
amefunguka kuwa
wanaomsema anatumia madawa ya kulevya ‘unga’, basi
wampeleke sober house (nyumba ya kusaidia waathirika wa unga) ili
akapatiwe tiba.
Akizungumza na 3-Tamu, Amber Lulu
alisema kuwa anavyojua teja wa unga huwa hajifichi hivyo kama kweli
anatumia, ipo siku itadhihirika kuliko kila siku kusemwasemwa juu ya
jambo ambalo hausiki nalo.
“Nimekuwa nikisemwa kila siku kuwa ninatumia unga, sasa nasema kama kuna mtu ana uhakika na hilo, basi anipeleke sober house nikatibiwe. Ni vyema watu wakajua kuwa hata mimi ni binadamu, ninaumizwa na kusemwasemwa,” alisema Amber Lulu.

Comments
Post a Comment