Msanii wa filamu na muziki Bongo, Baby Madaha Joseph.
MSANII wa filamu na muziki Bongo, Baby Madaha Joseph, amekiri kuwa kila mwaka hurudi kwao Mwanza kwa ajili ya
kuonana na wazee wake ‘kutambika’
ambao humsaidia kufanya mambo yake yaende vizuri mjini, kitu alichosema
ni muhimu sana katika wakati huu ambao maisha ni magumu.
Akizungumza na Za Motomoto News, Baby Madaha
alisema huwa anakwenda kwao kila mwaka na hivi sasa yupo huko kwa ajili
ya kuwaona wazee wa kimila kwani huwa wanamsaidia, hasa pale mambo
yanapokuwa magumu.
“Bila wazee mambo hayaendi kabisa, niko kwetu Mwanza kwa ajili ya
kufanya mambo ya kimila ili walau mambo yaende vizuri mjini maana hali
imekuwa mbaya sana, nimekuwa nikifanya hivyo kila mwaka na nimeona huwa
inasaidia sana,” alisema.

Comments
Post a Comment