Dar es Salaam. Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa
amewasili leo, Julai 20 saa
mbili asubuhi makao makuu ya Jeshi la Polisi
kwenye ofisi za Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI),
Robert Boaz.
Lowassa ameambatana na mkewe, Regina na mwanasheria wake, Peter Kibatala.
Hii ni mara ya nne kwa Lowassa kuripoti hapo
akituhumiwa kutoa kauli za kichochezi wakati wa futari iliyoandaliwa
Juni 23, na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.
Katika futari hiyo, Lowassa anadaiwa kutoa maneno ya
uchochezi kuhusu masheikh wa Taasisi ya Uamsho wanaoshikiliwa gerezani
akidai utaratibu wa kisheria ufanyike ili waachiwe huru.
Polisi wameimarisha ulinzi eneo hilo, huku Lowassa akiwa ndani tayari kwa kuhojiwa.

Comments
Post a Comment