Kagera .Rais John Magufuli amewasili katika uwanja wa
mpira wa Lemela Kata ya
Kanazi Wilaya Ngara Mkoani Kagera ambapo
atampokea Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza na baada ya hapo watakagua
gwaride.
Mara baada ya kumaliza ukaguzi wa gwaride hilo viongozi hao watakuwa na maongezi maalum.
Rais Magufuli yuko ziarani Kanda ya ziwa na jana alizindua barabara ya kiwango cha lami ya Kagoma- Biharamulo-Lusahunga.
Pamoja na uzinduzi Rais Magufuli pia alihutubia
wananchi ambako umati mkubwa umehudhuria uzinduzi wa barabara hiyo yenye
urefu wa kilometa 154.

Comments
Post a Comment