Mama huyo akinyanyuka kutoka kwenye ungo aliokuwa amekaa juu yake katikati ya barabara.
TUKIO la mama ambaye jina lake
halikupatikana mara moja kukutwa ameketi katikati ya barabara akiwa uchi
wa mnyama limezua tafrani na mjadala mkali kufuatia mazingira ya tukio
zima huku maswali yakiwa mengi kuliko uhalisia.
Kisanga hicho kilichozua taharuki na zogo kutoka kwa watu, kilijiri jana asubuhi maeneo ya Banana-Ukonga jijini Dar, hali iliyopelekea kusimama kwa shughuli za kijamii kwa muda.
…Akitokomea na mizigo yake baada ya watu kumshitukia.
MAZINGIRA YA TUKIO
Mapema asubuhi, wakati watu wakianza ‘mishemishe’ za kuikaribisha
siku mpya mama huyo alionekana ameketi katikati ya barabara, akiwa
mtupu na pembeni kukiwa na ungo na mkoba, jambao lililovuta hisia za
wengi na kulazimika kusogea karibu na eneo hilo kushuhudia kwa ukaribu
ili kubaini kilichojiri.
…Akizongwa na watu baada ya kuvaa nguo.…Akiwa ameshika ungo wake.
Ilizidi kudaiwa kuwa mama huyo alisikika akizungumza maneno
yasiyoeleweka huku akiwa na kiwewe akijaribu kutafuta namna ya
kujisitiri kuondokana na aibu. Kutokana na hali hiyo, baadhi ya akina
mama waliingiwa na moyo wa huruma kwa mwanamke mwenzao na kujitolea
mavazi (khanga) na kumsitiri ingawa wengine hususan wanaume walisikika
wakizomea na kushangilia huku wakimuita majina yenye tafsiri mbaya.
MJADALA ULIOZUKA
Katika eneo la tukio, yapo maswali makubwa matatu yaliyozua mjadala ambayo yalichangiwa na mazingira husika.
“Mbona mwanamke mwenyewe anaonekana mstaarabu wa kutoendana kabisa na
mazingira haya? Lakini pia kama ni mchawi au mwanga mbona anaongea
wakati ilivyo kawaida kama mchawi akinaswa akifanya uchawi wake huwa
hawaongei hadi ‘wagutuliwe’ tofauti na alivyoonekana mwanzo akizungumza
mwenyewe? Lakini pia mbona kuna mkoba, kwani mchawi huwa na mkoba
kweli?” Hayo ni baadhi ya maswali yaliyosikika kutoka kwa watu
waliokuwa eneo la tukio, huku yakizua mjadala na sintofahamu yenye fumbo
zito.



Comments
Post a Comment