Misri. Mahakama ya
Jinai ya Misri imewahukumu wanaharakati 43 wa
Kikundi cha Ikhwanul
Muslimin, kifungo cha maisha jela kwa madai ya kushiriki maandamano
dhidi ya Serikali.
Hukumu hiyo iliyotolewa jana na mahakama hiyo, imesema
wanaharakati hao walishiriki maandamano yaliyopigwa marufuku dhidi ya
Serikali, kuwashambulia maofisa usalama na kupora mali za umma wakati wa
maandamano hayo mnamo Desemba mwaka 2011.
Mbali na kuwahukumu kifungo cha maisha jela, mahakama
hiyo imewapiga faini washtakiwa hao ya Sh 2bilioni kwa madai ya kupora
mali za umma.
Wanaharakati wengine tisa wa Ikhwani wamehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela huku 92 wakiachiwa huru.
Baada ya Jeshi la Misri kumuondoa madarakani Mohammed
Morsi mwaka 2013, Serikali ya Cairo ilipiga marufuku shughuli zote za
wanaharakati hao.
Kadhalika idadi kubwa ya viongozi na wanachama wa
harakati hizo zilizopigwa marufuku wamefungwa jela na baadhi yao
wamehukumiwa adhabu ya kifo.

Comments
Post a Comment