Dar es Salaam. Kanisa la Ufufuo na Uzima lililopo Mbezi Inn linalomilikiwa na
Askofu Josephat Gwajima limebomolewa.
Nyumba hiyo ya ibada ambayo pia ilikuwa ikitumika kama kituo cha maombezi imebomolewa na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads).
Imeelezwa kanisa hilo limejengwa ndani ya hifadhi ya Barabara ya Morogoro ya mita 121.5.
Kwa mujibu wa waumini wa kanisa hilo, pia limekuwa
likitumika kama kituo cha kufundishia wachungaji limebomolewa jana
jioni hali iliyosababisha waumini wa Kanisa hilo kusalia nje.
Mwananchi imefika katika kanisa hilo na kukuta vitu vikiwa nje na baadhi ya waumini wakiendelea na maombi nje.
Mmoja wa waumini ambaye hakutaka kujitambulisha kwa
madai si msemaji, amesema kanisa leo limebomolewa lakini injili
inaendelea kuhubiriwa kama kawaida .
"Tunaendelea na huduma na kesho tutakuwa na ibada itakayoanza saa kumi jioni "amesema.
Muumini mwingine pia amesema hali ilikuwa mbaya jana
wakati kanisa hilo linabomolewa kwani waliwakuta wakiwa katika
maandalizi ya kufanya maombi.
Walifika jana wakatuambia tutoe vitu, ilibidi tuache
kufanya maandalizi tukatoa vitu" amesema muumini huyo huku akikataa
kutajwa jina kwa kuwa si msemaji mkuu wa kanisa hilo.

Comments
Post a Comment