WAZIRI wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),
George Simbachawene na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Edwin Ngonyani wameandika barua za kujiuzulu nyadhifa hizo ili kupisha
uchunguzi baada ya kutajwa kuhusika kashfa kwenye Ripoti za Uchunguzi wa
Biashara ya Madini ya Almasi na Tanzanite.
Uamuzi a viongozi hao umekuja baada ya
Rais Magufuli kupokea Ripoti hiyo kutoka kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
ambapo Rais aliwataka viongozi wote wa serikali walioko madarakani na
wametajwa kuhusika kwenye kashfa hizo waachie ngazi ili kupisha
uchunguzi wa vyombo vya usalama.
Kwa upande wake, akiongea leo Alhamisi
mchana mara baada ya hafla ya makabidhianao ya ripoti hizo, Ngonyani
amesema amepokea kauli ya Rais kwa mikono miwili na anaandika barua ya
kujiuzulu nafasi hiyo.
“Hata sasa unanichelewesha nipo
naandika barua ya kujiuzulu, hii ni nafasi niliyopewa na ni lazima
nimuunge mkono Rais katika hatua zake za kutaka kubadili mfumo wa nchi
na kuufanya wenye manufaa kwa wananchi,” amesema Ngonyani.
Amesema hawezi kuongeza chochote juu ya
kauli ya Rais na anaviachia kazi vyombo vya ulinzi na usalama kufanya
kazi yake kama ambavyo mkuu wa nchi amevitaka.


Comments
Post a Comment