Ni kama wanaigiliziana kwani baada ya
staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kumtelekeza baba
yake, Mzee Abdul Jumaa ingawa kwa sasa wako vizuri, msanii mwenzake,
Omary Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ naye ameingia kwenye mkumbo huo baada
ya baba yake mzazi, Faraji Nyembo kuibuka na kusema hata akifa asimzike,
Risasi Mchanganyiko limeelezwa.
Msingi wa madai ya baba Dimpoz ni kwamba mwanaye huyo hamjali na hajawahi kumjali kwa chochote kabla na hata baada ya kuwa staa
ATA LA DIMPOZ HUKO IBIZA
Kabla ya baba Dimpoz kufunguka ya
moyoni, uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kwamba, licha ya Dimpoz
kujiachia kwa kula bata sehemu maarufu za starehe duniani kama Ibiza
nchini Hispania akiwa na Mwanasoka wa Uingereza, Wayne Rooney, baba yake
anaishi mkoani Tabora katika lindi la umaskini, jambo ambalo
linawashangaza wanaoishi karibu naye.
“Hivi mna habari kwamba baba mzazi wa
Dimpoz ana maisha magumu sana huku Tabora? Kwa taarifa yenu huyu mzee
anaishi kwa kubangaiza kwenye Bajaj tofauti na jina alilonalo mwanaye
Dimpoz kwani ana jina kubwa ambalo ana uwezo wa kumsaidia baba yake,
akawa anaishi maisha mazuri yenye hadhi kuliko alivyo sasa.
“Ngoja niwatumie picha za baba Dimpoz
akiwa mtaani, akila mihogo na kachumbari kwa mamalishe maana ndiyo
maisha yake, si unajua maisha ya sasa wakati mwingine hata hiyo Bajaj
hailipi maana anaweza kukaa hata siku nzima hajapata mteja na huku
mkoani mambo ni magumu sana,” alieleza mmoja wa marafiki wa mzee huyo.
aada ya kupata habari hizo kwa kina, Risasi Mchanganyiko lilifanya
jitihada za kumpata baba wa Dimpoz na kufanikiwa kuzungumza naye ambapo
alieleza kwamba hawezi kumlaumu sana mwanaye ila anatakiwa ajue wajibu
wake kwa mzazi.
Alisema kuwa, anachojivunia ni kwamba
ameshamleta Dimpoz duniani maana hakuna kitu kikubwa kama kuletwa
duniani kwani asingemleta, basi hakungekuwa na mtu anayeitwa Omary
Nyembo.
“Hakuna kitu kikubwa duniani kama
kuletwa duniani…hayo mengine ya kwamba alilelewa na upande mmoja tu wa
mama, ni madogo tu hivyo sina kosa kwa kuwa nilishamleta duniani na
ninamshukuru Mungu ananipa nguvu ya kufanya kazi kwani nina Bajaj yangu
niliyonunua mwenyewe ninapambana na maisha, nina umri wa miaka 64,
lakini bado ninapambana.
AMTAJA WEMA SEPETU
“Ni kama Wema Sepetu anavyohangaika
kutafuta mtoto, siku akimpata hata kama hamsaidii chochote atamshukuru
tu Mungu hivyo na mimi huwa ninamshukuru Mungu maana nimeshamleta Omary
duniani.
“Yeye kama mtoto, ndiye anayetakiwa
kujua mzazi wake anahitaji nini, yaani ukimuuliza sasa hivi Dimpoz akupe
namba yangu, utaona, atakujibu nini maana ninaamini hana. Nimekuwa
nikimpigia, lakini simu yake unaambiwa inatumika, angekuwa anaona
umuhimu si angekuwa na namba maalum kwa ajili ya kuwasiliana na mimi
baba yake kama mastaa wengine wanavyofanya kuwa na namba kwa ajili ya
mashabiki na nyingine ya watu muhimu,” alisema baba huyo
NIKIFA ASINIZIKE
Baba Dimpoz hakuishia hapo kwani
aliendelea kutiririka kuwa, ikitokea siku ameaga dunia na Dimpoz
akatangaza au kwenda Tabora kwa ajili ya msiba, watu watamkimbiza kwa
kuwa hana ushirikiano nao na wanaona maisha anayoishi watamshushia
kipigo cha aina yake.
“Mfano nikifa kama leo ni bora huyo
Ommy asinizike au kuja Tabora maana watu watampiga na kwanza atasema ni
nani wake amefariki dunia maana hivi niko hai hana ushikiano,” alisema
baba huyo.
DIMPOZ ANASEMAJE?
Ili kuujua ukweli, naye anazungumziaje suala hilo, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta
Dimpoz ambapo simu yake iliita bila kupokelewa na alipotumiwa meseji
kwa njia ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp na kuelezwa madai hayo yote
kinagaubaga alijibu kwa kifupi: “Nipo hospitalini.”
Alipoulizwa kama anaumwa au anafanya
nini hospitalini, hakujibu na hata alipotakiwa kwenda kwenye hoja ya
msingi juu ya madai ya baba yake, pia hakujibu.
MASTAA WENGINE
Dimpoz anapita kulekule alikopita
Diamond na baba yake hivyo gazeti hili linamtaka kuyamaliza mambo hayo
na mzazi wake huyo kwani manung’uniko ya wazazi huondoa kabisa baraka
kwenye maisha ya mtoto.
Imeandikwa na Gladness Mallya na Sifael Paul.

Comments
Post a Comment